Breaking News

Ziara ya JPM Pwani yaanza na ahadi kibao

Rais John Magufuli

Rais ameyasema hayo leo, (Jumanne) wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Kibaha Mailimoja, katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

Pwani. Rais John Magufuli ameahidi kushughulikia suala la umeme na maji mkoani Pwani hivi karibuni.

Rais ameyasema hayo leo, (Jumanne) wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Kibaha Mailimoja, katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

Amesema Sh 30bilioni zitatumika katika mradi wa umeme mkoani humo.

Amesema kuna mradi wa maji Ruvu juu uliofadhiliwa na Serikali ya India, ambao maji yake yatatumika katika Jiji la Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo.

Rais amesema pamoja na mradi huo, pia kuna ujenzi wa bwawa la Kidunda, linalohifadhi maji ya mvua ili kukabiliana na upungufu wa maji nyakati za ukame.

No comments