Breaking News

Jose Mourinho naye yamkuta ya Cristiano Ronaldo

Wakati sakata la Cristiano Ronaldo kukwepa kodi likiendelea kupamba moto,mapya yameibuka ambapo kocha wa Manchester United Jose Mourinho naye amekumbwa na kashfa ya kuhusu kodi.

Ikumbukwe kwamba Mourinho na Ronaldo wote wanasimamiwa na wakala mmoja ambaye ni Jorge Mendez na sasa dunia imebaki kujiuliza kwa nini wateja wa Mendez wamekumbwa na kashfa inayofanana kwa kipindi kimoja.

Inadaiwa kwamba Jose Mourinho wakati yuko Real Madrid alifanya kosa kwa kukwepa kulipa kodi kiasi cha euro 3.3m,lakini sasa mamlaka zihusikazo na masuala ya kodi nchini Hispania zimegundua hilo na kuanza kufanya uchunguzi juu yake.

Ronaldo ambaye kama ilivyo kwa Mourinho ni Mreno inasemekana anaelekea kujiunga na Manchester United na kama dili hilo likifanikiwa baasi Manchester United kutakuwa na wakabiliwa wawili wa uhalifu wa ulipaji kodi.

Wakati Mourinho hayo yakimkuta, mtuhumiwa mwenzake ambaye ni Cristiano Ronaldo atahojiwa kwa mara ya kwanza kuhusu kesi yake siku ya tarehe 31 mwezi huu.

Cristiano Ronaldo ameanza kuhusishwa na kuhamia Manchester United ili kuikimbia ardhi ya Hispania ambako ndiko ambako moto wa kuhusu ukwepaji kodi unawaka kwa kasi kubwa sana.

No comments