Breaking News

Ufafanuzi wa Rais Magufuli kuhusu ile kauli ya kutoteua Wapinzani


Rais Magufuli leo Ikulu Dar es salaam amemuapisha Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ambaye Mwenyekiti katika chama cha ACT Wazalendo.

Baada ya kumuapisha, moja ya vitu alivizungumza Rais JPM ni kuhusu ile kauli yake ya kutoteua upinzani… kauli ambayo imekua ikisambaa kwenye video fupi baada ya kumteua Mama Anna Mghwira.

Leo Ikulu Rais Magufuli amesema ‘Siku zote nimekua nikisisitiza Tanzania kwanza, wapo wengine wanasema mbona ulishazungumza kuwa hutoteua upinzani? lazima watu waelewe nilizungumza hilo mahali gani…… nilizungumza hilo nikiwa Zanzibar

Pia msimamo wa kutoteua Mbunge wa Upinzani katika nafasi zangu 10 sitafanya hivyo kweli, nimeshateua 9 nimebakiza nafasi moja na hiyo nafasi moja haitokua ya Wapinzani’

JPM alimwambia Mama Mghwira >>> ‘Wapo watakaokuonea wivu wa kwenye chama chako, wapo watakaokuonea wivu ambao walitaka nichague tu kutoka CCM

Wapo watakaokuonea wivu hata wa CHADEMA sababu sikuchagua huko pamoja na kwamba wapo wengi wananiombaomba, mpaka Wabunge lakini nimesema hapana… nataka upinzani uwepo‘ – Rais Magufuli 

No comments