Breaking News

Tetesi za usajili: Ajibu ana ofa 3 Simba, Yanga, Singida UTD, ataenda wapi? 

 

brahim Ajib ameendelea kuwa gumzo kipindi hiki cha usajili, ametajwa kutaka kuondoka Simba ambao bado wanamtaka pia lakini wanatofautiana na mchezaji huyo katika dau la usajili.

Kwa taarifa ambazo www.shaffihdauda.co.tz inazo hadi sasa ni kwamba, Ajib na ofa tatu mezani kutoka Simba, Yanga na Singida United lakini mwenyewe bado hajafanya uamuzi kwamba atasaini katika klabu gani kwa ajili ya msimu ujao.

Inatajwa kuwa Simba imemuwekea Ajib kiasi cha shilingi milioni 50 ili asaini mkataba wa kuendelea kubaki katika klabu hiyo lakini yeye bado anataka vigogo hao waongeze mzigo ili aweze kusaini mkataba wao.

Kwa upande wa Yanga pia inasemekana amewekewa mzigo kama aliopewa Simba (milioni 50) kitu ambacho kina mfanya Ajib aone ni bora aendelee kubaki Simba kuliko kwenda Yanga kwa dau lilelile kama analotaka kulikimbia Msimbazi.

Watu wa karibu wa Ajib wanasema kwamba timu ya Singida United ndio timu pekee ambayo imetenga pesa ndefu kuliko Simba na Yanga kwa ajili ya kumnasa Ajib, Singida wameweka mezani kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 70 kwa ajili ya kuinasa saini ya Ajib.

Kama vile haitoshi, Singida United wako tayari kumlipa Ajib mshahara wa shilingi milioni tatu kwa mwezi wakati inasemekana Simba na Yanga zimeahidi kumlipa Ajib shilingi milioni mbili kwa mwezi.

Katika ofa hizo tatu Ajib bado hajaamua aende wapi hadi sasa licha kwamba jana Juni 13 kuna picha zilienea kwenye mitandao ya kijamii huku ikielezwa kwamba, Ajib amesaini mkataba na klabu ya Yanga lakini hakukua na uthibisho wa moja kwa moja kuhusu jambo hilo.

Vyanzo vyetu vimeendelea kutuarifu kwamba, licha ya ofa nzuri ambayo Singida United wameonesha kumpa Ajib lakini nyota huyo ana sita kukubali kwenda kujiunga na timu hiyo iliyopanda daraja kucheza VPL msimu ujao akihofia malengo yake ya kutoka kwenda kucheza soka nje ya nchi yanaweza yakachukua muda mrefu kufanikiwa.

No comments