Breaking News

Cristiano Ronaldo kwenda jela? mwenyewe ajibu “Quien no debe no teme”

Unakumbuka ile kesi ambayo ilimkumba Lioneil Messi na mamlaka za mapato za nchini Hispania hadi akapigwa faini ya euro 2m pamoja na kifungo cha nje? sasa kesi ile imehamia kwa mpinzani mkubwa wa Messi ambaye ni Cristiano Ronaldo.

Taarifa zinasema kwa muda sasa toka mwaka 2011 hadi 2014 nyota huyo wa timu ya Real Madrid amekuwa akikwepa kulipa kodi ambapo zaidi ya kiasi cha kodi cha euro 14m amekwepa kulipa katika kipindi hicho.

Tofauti na Lioneil Messi lakini kwa Ronaldo kosa lake ni kubwa sana kwani wapelelezi wa kesi yake wanadai mshambuliaji huyo alifungua hadi kampuni kwa jina jipya ili kukwepa kulipa kodi na kiasi ambacho Ronaldo amekwepa ni mara 3 ya kile kilichomtia Lioneil Messi matatani.

Messi kesi yake ilikuwa ni ukwepaji wa kodi kiasi cha euro 4.1m huku Cristiano Ronaldo ikiwa ni euro 16m, na Messi na baba yake walihukumiwa adhabu ya miezi 21 na faini ya euro 2m hali inayoonesha Ronaldo anaweza kukabiliwa na adhabu kubwa zaidi.

Ronaldo mwenyewe akizungumzia tukio hilo nchini kwao Ureno alipoulizwa na waandishi wa habari alijibu “Quien no debe no teme” akimaanisha “asiye na kitu cha kuficha hawezi kuogopa chochote” na akisisitiza haogopi kitu na ana uhakika wa kushinda kesi hiyo.

Sheria za masuala ya kodi nchini Hispania zinaweza kumuokoa Ronaldo asiende jela kwani kama hujawahi kupata kesi ya kulipa kodi hapo mwanzo au hujawahi kwenda jela na ikiwa ni mara yako ya kwanza kupata kesi kama hiyo baasi unatumikia kifungo cha nje ya jela.

 

No comments