Breaking News

Okwi Njoo Tuwanyooshe: Zimbwe Jr

Mshambuliaji Emmanuel Okwi.

BEKI wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’, amesema ujio wa Emmanuel Okwi utasaidia kuhakikisha wanafanya vizuri na kuzima utawala wa Yanga katika Ligi Kuu Bara. 

Msimu wa tatu mfululizo sasa, Yanga inatwaa ubingwa wa ligi kuu. Kutokana na hilo,  Simba sasa inajipanga kufanya vizuri msimu ujao na kuzima utawala wa Wanajangwani. Mara ya mwisho Simba kutwaa ubingwa huo ni mwaka 2012. 

Zimbwe Jr ambaye alipata kuwa maarufu kwa jina la Tshabalala, anaamini usajili unaoendelea kufanywa na uongozi wa timu yake utasaidia kuwapa mafanikio makubwa msimu ujao. 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Zimbwe Jr ambaye ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara na Mchezaji Bora wa Simba kwa msimu uliopita, alisema anafahamu uwezo wa Okwi raia wa Uganda, hivyo ujio wake utawasaidia kikosini. “Binafsi kwanza siyo mgeni na Okwi kwa sababu namjua vizuri, nimecheza naye Simba kabla hajaondoka, natambua uwezo wake sasa kuja kwake tena katika timu yetu itakuwa ni kitu kikubwa. 

“Muda mrefu tumekuwa tukisaka mafanikio kabla ya kubeba taji la FA, Okwi aje ili tuwe na timu bora ambayo itakuwa na uwezo wa kuifunga timu yoyote itakayokuja mbele yetu. “Naamini usajili unaofanywa na uongozi wetu utasaidia kuleta mafanikio makubwa ambayo Wanasimba wamekuwa wakiyatamani,” alisema Zimbwe Jr.

No comments