JE, Wanaoshangilia na Kupongeza Bajeti Wanajua Wanashangilia Nini?
Kwanza naomba na mimi nianze kwa kuipongeza bajeti na kuishangilia kwasababu tuu watu walipiga makofi, as when you are in Rome, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu walikuwa wakishangilia nini!. Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeji ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali kuhusu failures za utekelezaji wa bajeti tunazopanga kwa kutumia kitu kinachoitwa a common sense logic.
Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini au wanapongeza nini? . Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo imeshindwa kutekelezwa?!. Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, ukitokea wengi wa washangiliaji wakawa hawajui wanashangilia nini, ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi halafu watu wanashangilia?!. Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, tujue tushangilie nini?.
Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza, huku kuishangilia bajeti nakuita ni kuishangilia ujinga!.
Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu,;Jee Wanashangilia Bajeti, Wanajua Wanashangilia nini au ndio yale yale ya Kushangilia Chochote Bungeni.
Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wakijadili bajeti, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakikishi wetu wakichangia bajeti hiyo hivyo kututendea haki sisi wananchi
No comments