Zalio la vyeti feki ni CCM na serikali – Halima Mdee
Halima Mdee ametoka kauli hiyo, leo Mei 23, 2018 Bungeni jijini
Dodoma ambapo amesema kuwa kuna walimu/watumishi ambao wamelitumikia
taifa kwa miaka mingi sana, serikali inadhani ni sahihi kwa watumishi
hao kuondoka bila hata kuwapa kifuta jasho?
“Zalio la vyeti feki ni Chama cha Mapinduzi na Serikali yake, kwa
kipindi hicho tunafahamu kwamba walimu au watumishi wengi walianza na
cheti cha mtu wakaenda wakasomea taaluma wakafaulu taaluma zao wakaenda
kulitumikia Taifa hili kwa miaka mingi sana, serikali ya watu ni
serikali yenye ubinadam mi nataka niulize swali la nyongeza hivi kweli
serikali ya CCM inadhani ni sahihi kwa watu ambao wametumikia hili Taifa
kwa miaka 20 wengine mpaka miaka 40 wengine hata miaka 30 waondoke hivi
hivi bila hata kifuta jasho mnadhani ni sahihi.? amehoji Mdee.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Madini,Angellah Kairuki akijibu kwa
niaba ya Waziri wa TAMISEMI amesema kuwa “Nafahamu kuwa dada/Mdogo wangu
naye ni mwanasheria ‘You can make benefit for your own wrong’ suala
hili lilikuwa ni jinai huwezi ukanufaika hata kama uliweza kupenetrate
katika mfumo ikafikiwa hapo na Ndio maana Mh. Rais aliweza kutoa armnest
na hii haikuweza kutoka bure, kwahiyo Mh. Halima aweze kuelewa suala
hili halijazalishwa na serikali ya CCM ni criminal offence na ilikuwa ni
lazima kufanya hivyo.”
No comments