FA yaishushia rungu zito klabu ya Arsenal
Chama cha soka nchini Uingereza FA kimeipiga faini ya pauni 20,000
klabu ya Arsenal kufuatia wachezaji wake kumgasi mwamuzi baada ya
kuipatia penati timu ya Leicester.
Arsenal imelimwa faini hiyo ya pauni 20,000 kufuatia baadhi ya
wachezaji wake kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumgasi
mwamuzi, Graham Scott wakionyesha kutoridhishwa na maamuzi aliyofanya ya
kuwapatia Leicester penati dakika ya 75, kwenye mchezo wao uliyopigwa
Mei 9.
FA ameipatia adhabu The Gunners mapema mwezi huu baada ya idadi kubwa
ya wachezaji wake kumzonga mwamuzi huyo wakati akiwazawadia penati
Mbweha hao wa Uingereza ‘the Foxes’.
Kwenye mchezo huo Jamie Vardy alitupia bao huku Leicester wakiwa
nyumbani King Power Stadium wakifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3
– 1 dhidi ya Arsenal.
No comments