"Wakiacha tutabakana" – Musukuma
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Musukuma, amesema kwamba watu
wanaomsema Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuhusu watu
wasiojulikana na wanao likashifu jeshi la polisi na kulituhumu kwa mambo
yasiyofaa wanalikosea jeshi hilo, kwani bila wao tusingekuwa salam
Musukuma
ameyasema hayo alipokuwa KIKAANGONI East Africa Television, na kusema
kwamba iwapo jeshi la polisi likiacha kazi kufanya kazi hata kwa siku
moja hakutakuwa na amani, kwani watu watafikia hatua ya kubakana bila
kutongozana.
“Ilitengenezwa tu chuki kuwa watu wasiojulikana wanatumwa na Makonda,
sijui na nani!! Mara polisi, hii dhana si nzuri, haya matukio yametokea
sehemu nyingi, Kibiti huko, sijui wapi huko, ila mnalichafua tu jeshi
la polisi , Siku jeshi la Polisi likisema liache kufanya kazi, hali
itakuwa mbaya, hatutatongozana tutabakana.”, amesema Musukuma.
Sambamba na hilo Musukuma amesema watu wanaofanya hivyo hawako
sahihi, kwani badala yake wanapaswa kulishukuru jeshi hilo kwa jukumu la
kuwalinda wao na mali zao.
No comments