Breaking News

Inasikitisha Watoto wawili wa Familia Moja Wafariki Dunia Baada ya Kuangukiwa na Ukuta


Wakati mvua zikiwa zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha mafuriko, huko Jijini Mwanza watoto wawili wa familia moja wamefariki baada ya kudondokewa na ukuta kipindi mvua hizo zikinyesha zilizokuwa na upepo mkali.

Akizungumza kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wakati wakiwa wamelala katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.

Kamanda Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa Baraka (2) hukyu majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.

No comments