NJOMBE FC YAIONYA YANGA "MSITEGEMEE MTEREMKO TAIFA
LICHA ya kuhamasika kusaka ushindikwa udi na uvumba ili kupunguza wigowa pointi saba inazozidiwa na watanizao Simba, mabingwa watetezi, Yanga,wameambiwa na wapinzani waoNjombe Mji kuwa wasitarajie mteremkokatika Uwanja wa Taifa jijini Dar esSalaam leo.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwamkoani Njombe, mabingwa haowalipata ushindi wa bao 1-0 dhidi yawenyeji hao ambao walipanda darajamsimu huu sambamba na SingidaUnited na Lipuli FC.
Akizungumza na gazeti hili jana, KochaMsaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa,alisema kuwa huu ni wakati wa lalasalama na kilichoko katika mipango yaoni kushinda kila mchezo.
Nsajisgwa alisema kuwa kamawatashinda mechi zao zote zilizosaliaikiwamo dhidi ya vinara Simba na AzamFC, anaamini nafasi ya kutetea ubingwawanaoushikilia itawezekana.
Beki na nahodha huyo wa zamani waYanga inayodhaminiwa na Kampuni yaKubashiri Matokeo Michezoni yaSportPesa, alisema mechi zote za ligi ningumu na wamejiandaa kukabiliana naushindani kutoka kwa timu zote 16zinazoshiriki ligi hiyo.
"Wachezaji wetu wanafahamu ugumu naushindani uliopo katika ligi,tunawakumbusha kupambana katikadakika zote 90 kwa sababu tunaaminihakuna mechi nyepesi, kuhusumajeruhi, tunajua tutakavyoipanga timuna kila mchezaji aliyesajiliwa ana uwezowa kuitumikia Yanga," alisema kochahuyo.
Kwa upande wa Kaimu Kocha Mkuu waNjombe Mji, Mrage Kabange, alisemajana kuwa wamekuja Dar es Salaamkushindana na kuondoka na pointi.
"Haijalishi tunacheza ugenini, mpirahauna hivyo siku hizi, kikubwatunaifahamu Yanga na tumejipangakupambana nao uwanjani na si kuangalia ukubwa wa jina la klabu yao," alisema Kabange.
Baada ya mechi ya leo, Yanga itaendelea na maandalizi ya kuwakabili St Louise kutoka Shelisheli katika mchezo wa raundi ya awali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
No comments