Breaking News

NIMEACHANA NA DIAMOND KABISA SINA MPANGO WA KURUDIANA NAE TENA- ZARI


Zari Hassan maarufu Zari The Boss Ladyamesema hafikirii na hatarajii kurudiana namzazi mwenzake Naseeb Abdul 'Diamond'.

Zari aliyezaa watoto wawili na Diamondambaye ni msanii maarufu wa muziki ndanina nje ya nchi amesema hayo jana Februari23,2018 alipohojiwa na Shirika la Utangazajila Uingereza (BBC).

"Nilikaa muda mrefu nikafikiria vitu vingindipo nikasema unajua nininahitaji kufikiamwisho wa hili," amesema Zari alipoulizwaswali na mtangazaji Mariam Omary kuhusuujumbe aliouweka katika akaunti yake yakijamii ya Instagram akielezea kuachana namzazi mwenzake.

Alipoulizwa ulikaa na kutafakari ukaona ufikiehiliZari alijibu, "Tulikuwa tunajaribu kuonatuna-move kutoka  scandal (kashfa) ya kuwaamepata mtoto na tunaweza kusonga mbele."

"Lakini vitu kama hivi leo unasikia hivi leounaona vile sijui kukumbatiana na ma Xkwenye public, vitu vya kunidhalilisha,kunifanya nisiheshimike na watoto wangu,nimeachana naye kabisa," amesema.

Alipoulizwa iwapo Diamond alimpigia simukumuomba msamaha baada ya picha hizokusambaaZari amesema hakufanya hivyo nahakuona haja ya kumpigia simu kumuuliza.

Kuhusu Diamond kama atakwendakumwomba msamaha atakubali Zariamesema, "Si alishakuja kipindi  fulanialipozaa na huyo dada fulani (Hamisa Mabeto) sioni kama itawezekana."

Alipoulizwa iwapo Diamond atatuma watu wa kumwombea msamaha; Zari amesema hawezi kulizungumzia hilo kwa kujibu 'no comment'.

Zari alipoulizwa iwapo hilo la kuachana ni kutafuta kiki amejibu, "Yaani tumeachana kabisa, it's done. Sijui kama amekubali, tangu video zile zimetoka na X wake nimem-block wiki tatu hatuongei ndipo nika-post."

No comments