Breaking News

YANGA YAOMBA MECHI YAO NA KAGERA SIGAR ISOGEZWE MBELE


Klabu ya soka ya Yanga kupitia kwa msemaji wake Dismas Ten, imesema imedhamiria kuiandikia barua Bodi ya ligi kuomba kusogezwa mbele kwa mchezo wake  wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ten ameweka wazi hilo huku akitaja sababu kubwa kuwa ni ugumu wa ratiba unaoikabiri timu hiyo hivyo inahitaji kupata muda wa maandalizi ya mechi ya Ligi ya mabingwa Africa dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

''Tunatazama uwezekano wa kupeleka barua kwenye shirikisho au bodi ya ligi ili kuomba mechi yetu dhidi ya Mtibwa isogezwe mbele tuweze kujiandaa vizuri na mechi ya kimataifa, tunataka kushinda ili tufike mbali zaidi ya tulipoishia msimu uliopita'', amesema.

Yanga imeondoka jijini Dar es salaam kuelekea Songea kwenye mchezo wake wa kombe la shirikisho dhidi ya Majimaji na baada ya mchezo huo itaelekea Mtwara kucheza mchezo wa ligi na Ndanda FC Februari 28 kabla ya kurejea na kwenda Morogoro kucheza na Mtibwa Machi 3.

Yanga ambayo inashika nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa na alama 37, inatarajia kucheza mechi yake ya klabu bingwa Africa hatua ya kwanza Machi 6 dhidi ya Township Rollers kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.

No comments