Breaking News

NEC YAFUNGUKA JUU YA MWITIKIO MDOGO WA WANANCHI KATIKA KUPIGA KURA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imejibuhoja mbalimbali zinazotolewa na wadaukuhusu sababu zinazochangia mwitikiomdogo wa wananchi kujitokeza kupiga kuratofauti na idadi ya watu waliojiandikisha.

Ufafanuzi huo unatokana na idadi ya wapigakura waliojitokeza katika uchaguzi mdogo waubunge wa Kinondoni na Siha uliofanyikaFebruari 17 pamoja na chaguzi nyingine zahivi karibuni za ubunge na udiwani.

Katika Jimbo la Kinondoni kati ya wapigakura 264,066 waliojiandikisha ni wapiga kura 45,454 tu waliofika kupiga kura, huku Sihakati ya waliojiandikisha 55,313 waliopiga kurani 32,277.

Katika uchaguzi mdogo wa majimbo yaKalenga na Chalinze uliofanyika Machi 16, 2014, kati ya waliojiandikisha kupiga kura 71,964 ni 29,541 tu walijitokeza kupiga kurahuku Chalinze kati ya 92,000 walioandikishwawaliopiga kura walikuwa 24,422.

Pia, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 niwapigakura milioni nane pekee waliopigakura kati ya milioni 21 waliojiandikisha hukumwaka 2015, kati ya wapiga kura milioni 23.2walioandikishwa na waliojitokeza kupiga kurawalikuwa milioni 15.6.

Jana, Naibu Katibu Uendeshaji Uchaguzi waNEC, Irene Kadushi alijibu hoja mbalimbali zawadau akisema mwitikio wa wapiga kurawakati wa chaguzi ndogo hutofautiana nawakati wa uchaguzi mkuu na kitendo cha watu kuhama chama kimoja na kisha kuruhusiwa kugombea nafasi ile ile imechangia idadi ndogo ya wapigakura kwenye uchaguzi mdogo wa Februari 17. “Miaka ya nyuma tulikuwa na changamoto ya fedha katika kutoa elimu ya mpiga kura, lakini tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kutosha na sasa elimu ya mpiga kura ni endelevu. Hakuna taasisi yoyote inayoiingilia NEC katika utendaji wake ikiwemo Serikali ambayo jukumu lake huishia kwenye kuipatia tume fedha kwa ajili ya shughuli zake,” alisema.

Bosi huyo wa uchaguzi wa NEC alisema muundo wa tume hiyo unachangia wananchi kuwa na mtazamo kuwa wateule wa Serikali wanaosimamia uchaguzi kwenye ngazi za chini wanakipendelea chama tawala.

“Hii imepelekea (sababisha) sisi kuomba tupatiwe ofisi kwenye kanda mbalimbali hapa nchini jambo litakalotusaidia pia katika utunzaji wa vifaa vyetu vya kazi. Pia, tunataka tuwe na uwezo wa kuajiri wafanyakazi hasa wasimamizi wa uchaguzi hali itakayoiongezea tume kuaminika kwake,” alisema na kuongeza.

“Kikubwa ni watu waongeze uaminifu wao kwa tume ambayo imekuwa ikifanya kazi kubwa, kwani hata nchi ambazo tume zake zinaonekana ziko huru na haki bado zinalalamikiwa kwa mambo kadha wa kadha.”

No comments