Breaking News

WAZIRI MWIGULU ATAJA MATUKIO YALIYOMUUDHI SANA MWAKA 2017

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema kwamba katika matukio yaliyomuudhi sana mwaka 2017 ni pamoja na kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu pamoja na mauaji ya wananchi na Askari huko Kibiti.

Mh. Nchemba amesema hayo jana akiongea na waandishi mkoa wa Dodoma wakati akitoa muelekeo wa wizara yake kwa mwaka mpya wa 2018 nini kama wizara wamejipanga kufanya.

Mh. Nchemba amesema kuwa matukio hayo yalimuudhi sana,  hivyo amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa na wao kama wizara wapo vitani mda wote kuwasaka wahalifu na kuzuia uhalifu kwa mwaka 2018.

Aidha Waziri Nchemba amewataka wananchi kutokuchukulia kawaida taarifa za kupotea kwa watu zaidi ya wiki bila kutoa taarifa kwa kudhani kuwa atakua mahali fulani, au hakuna ubaya unaoweza kutokea na hata wale wanaopewa vitisho wasichukulie kirahisi mambo hayo bali watoe taarifa polisi.

Akizungumzia kuokotwa kwa miili ya watu katika fukwe za bahari Dk. Nchemba amesema kwamba, miili  hiyo ilikua ya wahamiaji haramu amabao walikuwa wanasafirishwa nje ya nchi na wahamiaji hao walikuwa wanasafirishwa katika magari yasiyo na  hewa na wanabebwa kama mahindi, na kuogeza kuwa wakifa kwa kukosa hewa na chakula basi hutupwa sehemu mbalimbali ili wanaowasafirisha wasikamatwe.

No comments