Breaking News

DKT SHIKA AFUNGUKA KWENDA MAREKANI KUFANYA KAZI UN

Mtanzania Dkt. Louis Shika amedai mara baada ya kumaliza mambo yake hapa nchini anatarajia kwenda nchini Marekani kufanya kazi Umoja wa Mataifa (UN) ambapo aliteuliwa kuwa balozi miaka mitatu iliyopita.

Dkt. Shika amekiambia kituo cha runinga cha Azam kuwa anachoshughulikia kwa sasa hapa nchini ni kuingiza fedha zake zilizopo nje ya nchi ili awe kufungua kampuni na itakapoanza kufanya kazi ndipo atasafiri.

“Basi nitakuwa nimemaliza kazi yangu kwa hapa Tanzania ninaondoka kwenda Marekani kuitumikia dunia, mimi ni balozi katika Umoja wa Mataifa uteuzi ambao ulifanywa 2014 na sikuripoti kazini lakini hawajakata tamaa miezi miwili iliyopita nimepandishwa cheo kwa ngazi ya juu,” amesema Dkt. Shika.

“Mwanzo niliteuliwa kuwa balozi wa wakimbizi kwa upande wa Afrika, sasa nimechaguliwa kuwa balozi wa wakimbizi ulimwenguni kote, kwa hiyo ofisi kutoka Nairobi inahama kwenda New York,” amesisitiza.

Utakumbuka umaarufu wa Dkt. Shika ulikuja baada ya kujitokeza katika mnada wa  kuuza nyumba za Lugumi ambapo aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800, kisha kudai anangojea fedha zake kutoka nchini Urusi.

No comments