MPANDA MAJENGO MAREFU MAARUFU NCHINI CHINA AFARIKI DUNIA WAKATI AKIONESHJA UTUNDU WAKE
Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.
Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.
Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.
No comments