Breaking News

JESHI LA TANZANIA KUENDELEA KULINDA AMANI DR CONGO LICHA YA KUPOTEZA WANAJESHI 14


Jeshi la Tanzania kuendelea kulinda amani DR Congo licha ya kupoteza Wanajeshi 14
-
Hatua hii itaimarisha uhusiano wa kidiplomasia pamoja na shughuli za kibiashara
-
Wiki iliyopita wanajeshi 14 wa Tanzania na 5 wa DR Congo waliuwawa na wengine zaidi ya 44 walijeruliwa katika shaumbulio linalotajwa kuwa baya tangu mapigano dhidi ya waasi yaanze katika ukanda wa mashariki mwa nchi hiyo hasa eneo la Kivu ambalo kwa sehemu kubwa linazungukwa na makundi ya waasi.
-
Kwa mujibu wa Umoja wa Taifa (UN) unasema shambulio hilo lilitokea Desemba 7 mwaka huu katika kambi ya jeshi ya ulinzi wa amani (MONUSCO)
-
Waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) walivamia kambi ndogo iliyopo eneo la daraja la mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamanga mpakani mwa Uganda Kaskazini Mashariki ya Wilaya ya Beni, jimbo la Kivu Kaskazini
-
Siku chache baada ya shambulio hilo serikali ya Tanzania kupitia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema shambulio hilo limeleta madhara makubwa lakini kikosi chao kilichopo huko kina uwezo wa kutekeleza majukumu kwa uweledi na umahiri stahiki.

No comments