Breaking News

MATOKEO MABOVU YA KILI STARS JULIO KASHINDWA KUYAVUMILIA


Kama unavyofahamu Kilimanjaro Starsimetupwa  nje ya kombe la Chalenji hukuikiwa haijashinda hata mchezo mmoja kati yaminne iliyocheza kwenye kundi lake lililokuwana timu tano. Tanzania ilipoteza mechi zaketatu (Tanzania bara 1-2 Zanzibar, Rwanda 2-1 Tanzania bara, Kenya 1-0 Tanzania baranakutoka suluhu katika mechi moja (Libya 0-0 Tanzania bara).

Kocha mzoefu Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ambaye kwa sasa anafundisha Dodoma FCinayoshiriki ligi daraja la kwanza matokeowaliyopata Kili Stars kama wangepata vijanawa Serengeti Boys ‘sasa Ngorogoro Heroes’waliocheza AFCON U17 hakuna mtu ambayeangeshangaa kwa sababu tungesematunawapa uzoefu vijana.

Julio  pia amegusia suala la kocha AmmyNinje kupewa timukwa upande wakeamesema, hana tatizo na kocha huyoisipokuwa inawezekana hana uzoefu wakutosha kufundisha timu ya taifa ukizingatiaamekaa nje ya nchi kwa muda mrefu hivyoinawezekana anakosa uzoefu kwa wachezajiwa kibongo na tamauni zao.

“Mimi simpingi Ammy ni kijana wangu naalikuja kucheza kwenye timu ya taifalakinikwa jinsi alivyoishi huko hatujui kazi yakekubwa aliyokuwa anafanya ingawainasemekana ni kocha wa vijana lakinitusiamini kila mtu kwa kipindi hikitulichonachoWachezaji wetu wanahitajikumzoea mtu kulingana na mazingira,anaweza kuja mtu akawa na style yake halafuwachezaji wakashindwa kwenda nayo kwakipindi hicho kifupi cha mashindano.”

“Lakini kama suala la muungano si yupoMecky Maxime ambaye ndio alikuwa kochabora, unapokuwa kocha bora maana yakeniniUnapokuwa kocha bora inawezekanajeusiwe kocha wa timu ya taifa. Uongozi wa TFF uliopita ulikuwa na ukiritimba na chuki ya kukataa watu fulani kwa sababu ya faida zao sasa hivi naona TFF ina watu ambao tunategemea wanabusara na ueledi mkubwa watu kama Kidao amecheza mpira sasa hivi ni Kaimu Katibu wa TFF, Msafiri Mgoyi ni muumini wa timu za vijana.”

“Nilitarajia matokeo haya tungeyapata kwa timu yetu ya Serengeti Boys kwa sababu tungekuwa tunatengeneza exposure kwa vijana lakini tunapeleka timu hiyohiyo wachezaji ambao kila siku tunafungwa. Tungepeleka watoto tungesema tunawapa uzoefu lakini tumepeleka wakubwa ambao ndio tunawategemea kwenye mashindano yote lakini bado tumefungwa.”

“TFF waangalie kwa umakini mkubwa sio tunaaminia tu kwa sababu ambazo wanazijua wao mwisho wa siku Ammy anarudi Uingereza aibu inakuja kwetu. Tatizo halianguki kwa Ammy inaonekana TFF wakosefu hakuna makocha wa kufanya kazi.”

Kuna wakati Julio na Charles Boniface Mkwasa walikuwa makocha wa timu ya taifa, lakini jambo ambalo si la kutegemewa wachezaji wao waliwahi kuzomewa na mashabiki kutokana na matokeo mabovu, Julio ametoa ufafanuzi juu ya hilo.

“Mimi nimefundisha Simba, Mkwasa amefundisha Yanga kwa bhiyo tunapokuwa na wachezaji wa Yanga watatu, Simba saba kwa sababu yupo Julio, wachezaji wa Simba watazomewa lakini wakiwa wa Yanga tisa wa Simba watatu wa Yanga watazomewa. Hatuwezi kufika, na wapenzi wa soka ndio tunasababisha hali hii, turudi kwenye wakati ule aliokuwepo Marcio Maximo wakati timu inahamasishwa na na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.”

“Rais Kikwete alikuwa analipa makocha na aliupenda mpira kwa kiasi kikubwa, kama tungempa support kubwa leo tungfekuwa mbali sana kwenye soka lakini mchango wote wa Kikwete umepotelea hewani bila kujijua matokeo yake leo tunahangaika.”

“Ninaimani TFF mpya iliyoingia kama wanataka kumpa timu kocha mzawa kama vile Mayanga basi apewe stahiki zote zinazostahili ambazo angepata kocha mzungu lakini ukimnyima inakuwa  tatizo na wapenzi nao wai-support timu yao ya taifabila kujali huyu Yanga wala Simba maana ndio siasa za mpira wan chi hii kinyume cha hapo hatuwezi kupata mafanikio ndio maana unaona timu yetu inaenda hovyo.”

“Wachezaji wetu lazima wajitoe bila kujitoa hatuwezi kupata mafanikio, angalia Zanzibar siku zote tukicheza nao, mimi nikiwa mchezaji wa timu ya taifa tumecheza na Zanzibar mara mbili, moja Uganda wakawa mabingwa marea ya pili Malawi zote walitufunga goli mojamoja kwa sababu wachezaji wa kizanzibar wana commitment wanapotaka kushindana matokeo yake leo wanaonekana wanatumia dawa za kusisimua misuli. Kwa hiyo tujifunze kutoka kwao.”

Hatua ya makundi ya Challenge Cup imehitimishwa jana jioni ambapo tayari timu nne zilizofuzu hatua ya nusu fainali zimeshajulikana na zilizoaga mashindano tayari zinafahamika. Zanzibar walipoteza mechi yao kwa kufungwa 1-0 na Libya lakini wamefanikiwa kupenya kucheza nusu fainali ambapo watacheza dhidi ya Uganda (mabingwa watetezi) siku ya Ijumaa.

No comments