HATIMA YA SCOPION KUJULIKANA MWAKANI HUKUMU YAKE KUSOMWA JANUARI 10
Kesi ya kumjeruhi mpaka kumtoboa machokinyozi Said Mrisho inayomkabili mwalimuwa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msaniiwa filamu za kibongo, Salum Njwete maarufuScorpion hatimaye imefikia tamati ambapohukumu inatarajiwa kusomwa januari 10mwakani.
Kesi hiyo iliendelea jana katika mahakama yaHakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Darambapo Scorpion alikuwa akibanwa maswalina wakili wa utetezi, Nassoro Katuga kufuatiautetezi wake alioutoa kipindi kilichopitaakiongozwa na wakili wake, Juma Nassoro.
Katika utetezi wake wa awali Scorpionalisema alishurutishwa kutoa maelezo katikakituo cha polisi cha Buguruni ambapo wakiliKatuga alimuuliza kwanini alisaini.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haulealiifunga kwa kuahidi kuitolea hukumuJanuari 10 mwakani ambapo kabla yahukumu hiyo kesi hiyo itatajwa tenamahakamani hapo Desemba 27 mwaka huu.
No comments