BABU SEYA APATA PIGO LINGINE
SIKU chache baada ya Babu Seya na Papii Kocha kuachiwa huru kutokana na kupewa msamaha wa rais Magufuli, familia hiyo imepata pigo baada ya mdogo wa Babu Seya aitwaye Crizo Chimbukizi kufariki dunia.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, King Kikii, Crizo alifariki dunia jana kutokana na mshtuko wa moyo baada ya kupewa taarifa ya kuachiliwa huru kwa wawili hao na kwamba taratibu za mazishi zinafanywa.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa mkoa wa Katanga Kongo nyumbani kwa familia ya Nguza.
No comments