Breaking News

RAIS MAGUFULI ANG'ARA UINGEREZA


Viongozi wa Chama Cha Labour nchini Uingereza wamepongeza jitihada za Serikali ya CCM ya awamu ya Tano Chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuwa madhubuti katika vita dhidi ya rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na kutetea haki ya watanzania katika

Salamu hizo kutoka Chama Cha Labour zimetumwa kupitia Katibu wa NEC Mwenye dhamana ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg . Ngemela Lubinga katika Mkutano Mkuu wa Chama rafiki cha Labour na CCM.
Akiwakilisha salamu za Rais  Magufuli, Mwenyekiti wa CCM katika mkutano huo Ndg. Lubinga amesema kwamba ni lazima vyama rafiki hasa vyenye mrengo wa kijamaa kusimama pamoja katika kuhakikisha usawa na haki linapokuja suala la uvunaji wa rasilimali madini hasa katika nchi za Afrika.

          

                                                              
Ndg. Ngemela Lubinga alijulisha viongozi hao kuwa CCM inaendelea kufanya Mageuzi Makubwa ambayo lengo lake ni kurejesha Chama katika misingi yake na kuimarisha kwa vitendo uhalisia wa kwamba CCM ni Chama Cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu.
"Kama sehemu ya Mageuzi haya ndani ya Chama na katika Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeielekeza Serikali kutoa elimu bure kutoka darasa la kwanza mpaka kidato cha nne na kuongeza maradufu mikopo kwa wanafunzi wote wenye uhitaji wanaosoma katika vyuo vikuu nchini" Lubinga

Akihitimisha salamu za CCM katika Mkutano huo Mkuu wa Chama Cha Labour, Ndg. Lubinga Amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha labour kuweka maslahi ya umma mbele na kushughulika na changamoto zao ikiwemo mahusiano ya Nchi ya Uingereza na Jumuiya ya Ulaya.
Katika Mkutano huo Chama cha Labour kimeweka mikakati ya kurejesha Chama hicho katika kushika hatamu ya uongozi nchini Uingereza.


No comments