Breaking News

Nape Nnauye Ashtushwa na Mapendekezo ya Serikali

Mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye amedai kwamba ameshtushwa sana na mapendekezo ya serikali kuhusu kuwekeza pesa kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara.

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye
Akichangia leo Bungeni kwenye mjadala wa kujadili Mpango wa Taifa , Mh. Nape amesema kwamba baadhi ya miradi ambayo ingeweza kutekelezwa na sekta binafsi ni ujenzi wa reli ya kisasa ya kati, mradi wa umeme Rufiji, mradi wa bandari na uboreshaji shirika la ndege.
Nape amesema kwamba aliposoma mapendekezo alishtuka baada ya kuona kwamba Serikali inapendekeza kuwekeza pesa za Serikali kwenye miradi ambayo inaweza kuendeshwa kibiashara ambayo pia watu binafsi wangeruhusiwa kuiendesha.
"Kama mpango huu utatekelezwa kama ulivyo, miradi hii inakwenda kuuwa uchumi wa nchi yetu. Miradi hii mikubwa inaweza kujiendesha kibiashara na ikajilipa yenyewe, Niweke rekodi sawa Sipingi kutekelezwa kwa miradi   mikubwa ila napingana na Serikali jinsi ya kuifadhili na kuiendesha kwa kutumia fedha za Serikali" Nape
Akiendelea kusimamia hoja yake Mh. Nape amesema kuwa miradi hiyo ni mikubwa na itagharimu fedha nyingi ambazo zitailazimisha Serikali kukopa fedha nyingi, hali ambayo itaathiri deni la taifa ambalo kwa sasa Dola bilioni 26.
“Serikali ikienda kukopa na kwa sababu miradi hii inachukua muda mrefu maana yake tutaanza kulipa deni kabla ya miradi hiyo haijaanza kurudisha faida kwa taifa. Kwanini tunataka kung’ang’aniza kuchukua pesa ya Serikali”. Hebu tufikirie upya. Dk Mpango rudini mkafikiri upya”  Nape
Nape ameongeza kwamba "Huu mpango wako mzuri lakini rudini kwenye mawazo ya kutumia sekta binafsi. Tukienda hivi tunaenda kuua uchumi,”alisema

No comments