Breaking News

HOTEL KUBWA DAR YAFUNGWA KWA KUDAIWA BILLIONI 5.7


Hoteli ya Blue Pearl iliyoko eneo la Ubungo Jijini Dar es Salaam, imefungwa na kampuni ya Udalali ya Yono kutokana na mmiliki wake kushindwa kulipa kodi ya pango inayodaiwa na Ubungo Plaza.

Kampuni ya udalali ya Yono imeifungia hoteli hiyo pamoja na kuliondoa jina la hoteli katika jengo Ubungo Plaza mapema leo asubuhi, Novemba 9, majira ya saa 12 aubuhi, huku wateja waliokuwamo katika hoteli hiyo wakilazimishwa kuondoka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastika Kevela amesema hoteli hiyo inadaiwa kodi ya pango na Ubungo Plaza ya shilingi 5.7 bilioni.

“Tunafunga na kukabidhi kwa mmiliki na shughuli hapa hazitaendelea tena hadi awe amelipa kodi,” amesema Kevela.

Wateja waliokuwamo katika hoteli hiyo wamelalamikia usumbufu walioupata wa kuamshwa na kutakiwa kuondoka hotelini hapo aubuhi na mapema licha ya kuwa wamelipia gharama za kuwepo hotelini hapo.


No comments