Breaking News

Ben Pol Alamba Shavu la Ubalozi Ufaransa


Msanii wa muziki wa R&B, Ben Pol ametua nchini Ufaransa katika mji wa maraha, Paris kwaajili ya kuhudhuria halfa maalumu iliyoandaliwa na taasisi ya Maua.

Muimbaji huyo amedai katika halfa hiyo itakayofanyika tarehe 18 mwezi huu atatangazwa kuwa balozi wa taasisi hiyo inayojihusisha na kusaidia watoto katika mambo ya afya.

“Jana niliwasili mjini Paris (France) kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalum iliyoandaliwa na taasisi ya MAÜA Association, itakayofanyika tarehe 18 Novemba 2017 mjini humu.
Hafla hiyo itaambatana na utambulisho rasmi wa BenPol kama balozi mpya wa MAÜA association.,” aliandika Ben Pol Instagram.

“Sherehe hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Wana-diaspora, viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,”

“Maüa association (MAÜA) ni taasisi iliyoundwa na kusajiliwa nchini Ufaransa kwa minajili ya kutoa usaidizi wa kiafya kwa watoto na vijana ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao. #feelingood #feelingloved#godbless ,” aliongeza muimbaji huyo.

Hata hivyo muimbaji huyo hakuweka wazi ubalozi huo utamnufaisha kwa namna gani.

No comments