Breaking News

ACT WAZALENDO WAGOMA KUPEKULIWA

Polisi wamefika Makao Makuu ya ACT, wamekutana na Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu, ambaye baada ya kuwapokea amewaeleza kuwa mwenye Ofisi ni Katibu Mkuu ambaye hayupo ofisini.

Amewaeleza pia kuwa kama Jeshi la Polisi lilitaka kufanya Upekuzi kwenye Ofisi za ACT Wazalendo, nafasi nzuri kwao ilikuwa ni jana kwa kuwa walimhoji Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo kwa Masaa 7.

Polisi wamesisitiza kufanya upekuzi leo, hivyo wameamua kumfuata Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, nyumbani kwake ili awepo wakati wa upekuzi husika.

No comments