Breaking News

Picha 15: Athari zilizosababishwa na mvua Dar es Salaam

Oktoba 25 na 26 mvua kubwa imenyesha katika maeneo mbalimbali nchini ambapo katika Jiji la Dar es Salaam ni moja wapo ya maeneo ambapo imenyesha sana.

Kutokana na ubovu au kutokuwepo kabisa kwa miundombinu ya maji, mvua inaponyesha Dar es Salaam madhara mbali hutokea ikiwa ni pamoja na wananchi kuharibiwa mali zao kutokana na maji kuingia ndani, watu kufariki dunia, kukosekana kwa huduma mbalimbali hasa ya usafiri, kulipuka kwa magonjwa yakiwemo kipindupindu.

Mtu mmoja jijini Dar es Salaam anahofiwa kupoteza maisha kutokana na mvua hiyo iliyonyesha, lakini pia Oktoba 26 huduma ya usafiri ya mabasi yaendayo haraka ilisimamishwa kwa muda kuanzia saa 7:30 mchana kutokana na kufungwa kwa Barabara ya Morogoro kwa sababu ya Daraja la Mto Msimbazi lilijaa maji.

Hapa chini ni picha zilizopigwa kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam zikionyesha athari za mafuriko baada ya kunyesha kwa mvua hiyo. Picha zote na Iman Nsamila















No comments