MKEMIA MKUU KUCHUNGUZA GONGO ILIYOUA DAR
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa taarifa kuhusiana na vifo vya watu 10 vinavyodaiwa kutokana na unywaji wa gongo, anaandika Charles William.
Vifo hivyo vilivyotokana na watu hao kunywa gongo ambayo ni pombe ya kienyeji isiyoruhusiwa hapa nchini, viliripotiwa kutokea tarehe 3 na 4 Oktoba mwaka huu katika hospitali ya Tumbi na Mwananyamala huku watu wengine wakifa nyumbani kabla ya kupelekwa hospitali.
Hii ni taarifa kamili ya polisi iliyotolewa leo.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam mnamo tarehe 04/10/2017 majira ya saa kumi kamili alfajiri lilipokea taarifa kutoka kwa mwananchi aitwaye MATIGO RAMADHANI (38) mkazi wa Kimara Stop over kuwa tarehe 03/1
No comments