Lema Aiweka Mtegoni TAKUKURU
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema kwamba jambo la kupeleka ushahidi Takukuru tatizo siyo rushwa kutumika bali ni mambo mengine makubwa yaliyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali ikiwepo kuchoma shule kwa ajili ya kujipatia madaraka.
Akifanya mahojiano na EATV, Lema amesema kwamba kupitia video walizorekodi kuna video inamuonyesha diwani aliyenunuliwa akizungumzia kuwa aliyekuwa akichoma moto shule za Arusha ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda.
"Kwangu kuchomwa shule moto ni jambo la muhimu kuliko Rushwa iliyotumika kununua madiwani Arusha. Hii inahusisha watoto kuungua na mauti. Ikifika mahali watu tunataka madaraka kwa kiasi hicho inakuwa hatari. Sijasema amefanya lakini najaribu kufikiria kama ni Lema ningekuwa nimeonekana nikitoa rushwa kwa ajili ya kununua madiwani au balozi sijui Mkurugenzi wa Takukuru angechukuaje hatua kuhusu mimi. Nachotaka ni kuona haki na sheria inachukuliwa" amesema Lema.
Ameongeza kwamba, hata kama baada ya kukabidhi ushahidi wao hatua stahiki zisipochukuliwa kwa watuhumiwa anaamini tayari wao kama viongozi waliofanikisha shughuli hiyo watakuwa wamekwisha timiza majukumu yao na kuwataka kila mwenye nafasi ya kufichua maovu afanye
"Wenye mamlaka wakiona kwamba siyo jambo la msingi na wakaamua kupuuza sisi htutakuwa na la kufabnya isipokuwa tunawaachia wao na sisi tutakuwa tumekamilisha wajibu. Tunaamini ipo siku na hiyo siku ipo karibu sana hao wananchi wanaonekana kuwa ni wapuuzi watakuwa ni watu wenye akili sana" Lema ameongeza.
No comments