Ndizi ni miongoni mwa tunda lenye ladha nzuri na hupendwa na watu wengi katika nchi mbalimbali hapa ulimwenguni ikiwemo Tanzania, ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalam kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ na vile vile ina kiasi kingi cha nyuzi yaani 'fiber' ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni.
Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza na kuimarisha nishati ya mwili, ambapo pindi ulapo tunda hili unaweza kupata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakuwa umekula ndizi mbili tu na kwa sifa hiyo tunaweza kusema ndizi huenda likawa tunda muhimu sana pia kwa wanamichezo.
Hata hivyo, nishati siyo faida pekee unayoweza kuipata katika ndizi kwani pia ni tunda lenye uwezo wa kuponya na kuzuia matatizo mengine ya kiafya likiwemo suala la mfadhaiko wa akili (depression)
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha Afya ya Akili cha Taifa (MINDI) cha nchini Uingereza kwa watu wanaosumbuliwa na tatizo la mfadhaiko wa akili, watu wengi waliondokana na tatizo hilo na kujisikia vizuri baada ya kula ndizi mbivu. Hali hii inatokana na ukweli kwamba ndizi huwa na kirutubisho kinachojulikana kama ‘tryptophan,’ ambacho ni aina fulani ya protini inayotumika mwilini kumfanya mtu kuwa mtulivu na mwenye furaha.
Hali kadhalika, ndizi pia huwasaidia wanawake wanaopata matatizo wakati wa hedhi, hivyo endapo wewe ni miongoni mwa wale akina mama wanaopatwa na matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa hedhi, unashauriwa kula ndizi mbivu na unaweza kuponywa.
Mbali na kusaidia wakina mama katika matatizo ya hedhi pia ndizi huweza kuwasaidia watu ambao husumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu (anemia), hii ni kwasababu ndizi imekuwa ni chanzo kizuri cha madini ya aina ya chuma (iron), hivyo inaweza kuwa ni dawa ya kuzuia na kuponya tatizo la upungufu wa damu kwasababu madini ya chuma huamsha uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini.
Ama hakika tunda hili ni la kipekee kwani pia huweza kusaidia kukabiliana na tatizo la shinikizo la damu kwani lina kiwango kikubwa cha madini ya ‘potassium’ na wakati huo huo pia tunda hili lina kiasi kidogo cha chumvi ‘sodium’ na hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu na katika kuonesha uwezo wa tunda hili juu ya kusaidia kukabilina na shinikizo la damu ni pale ambapo miaka ya hivi karibuni Mamlaka ya Dawa na Chakula ya nchini Marekani iliamua kuwaruhusu wazalishaji na wauzaji wakubwa wa ndizi nchini humo, kutangaza rasmi uwezo wa ndizi katika kupambana na hatari ya shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (stroke) kwa binadamu.
Lakini mbali na hayo pia hivi karibuni wanafunzi wapatao 200 katika shule ya Twickenham nchini Uingereza, waliweza kufaulu mitihani yao kwa kula chakula cha mchana, ambapo inaelezwa kuwa ndizi ziliongeza uwezo wao wa kufikiri. Hii ni kwasababu utafiti unaonesha kuwa 'potassium' inayopatikana kwa wingi katika ndizi inaaminika kuwa na uwezo wa kumsaidia mwanafunzi kuamsha uwezo wake wa kufikiri zaidi.
Sambamba na faida hizo za tunda hili pia inaelezwa huweza kusaidia kupunguza Kasumba yaani 'hangovers' ndizi ni moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unaotokana na ulevi wa jana yake (hangovers) , hivyo unaweza kunywa ‘milk shake’ iliyotengenezwa kwa ndizi na kutiwa asali. Ndizi hutuliza tumbo ikisaidiwa na asali, inayorejesha kiwango cha sukari kilichopungua kwenye damu wakati maziwa nayo hutuliza na kurejesha maji kwenye mfumo wake.
Pamoja na hayo ndizi pia husaidia katika matatizo mengi na kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasi wasi, kutuliza vidonda vya tumbo, tindikali na kushusha joto mwilini pamoja na kurekebisha mapigo ya moyo. n.k.
Hivyo, ndizi ni tiba ya magonjwa mengi na ni bora kwa afya yako na endapo utatumia tunda hili vizuri,
No comments