Diamond Platnumz ameshitakiwa
Muimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz jina lake linazidi kuchukua headlines baada ya kuripotiwa kuwa amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mabetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
Wakili Zulu amesema kuwa mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba, kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30 2017.
No comments