Breaking News

JPM kutoshiriki kumbukumbu ya Nyerere


 

Taasisi mbalimbali za umma na zisizo za umma zinazomualika Mhe. Rais katika shughuli za kumbukumbu ya Mwl. Julius Nyerere zinakumbushwa kutokutangaza ushiriki wa Mhe. Rais Magufuli katika shughuli zao mpaka zipate uthibitisho kutoka Ofisi ya Rais

Taarifa iliyotolewa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli hatakuwa mgeni rasmi katika kongamano la maadhimisho ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kama inavyotangazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Aidha taarifa hiyo imeongeza kwamba Oktoba 11, 2017 ambayo inatangazwa kuwa ndio siku ya kufanyika kwa kongamano hilo, Mhe. Rais atakuwa na majukumu mengine ya Kitaifa kulingana na ratiba yake ya kazi na kuwataka watu wote kuzingatia utaratibu.

No comments