Tumeshinda Tumeshinda' Ndio Ujumbe wa Tundu Lissu Kwa Zitto Kabwe
sasa zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuvamiwa na watu wasiojulikana kisha kupigwa risasi September 7, 2017 Dodoma kisha kupelekwa Nairobi kwa ajili ya matibabu huku hali yake ikielezwa kuwa nzuri.
Watu mbalimbali na wanasiasa hasa wa CHADEMA wamekuwa wakimtembelea Hospitalini hapo kujua hali yake na mmoja kati ya waliomtembelea ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye baada ya kuonana naye alimwambia maneno ambayo Zitto aliayaandika kupitia kupitia Facebook yake.
Ujasiri ni nini ?
Nimetumia wikiendi iliyopita kumsabahi ndugu Tundu Lissu jijini Nairobi. Nimerudi nikiwa mwenye unyenyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao kaka yangu ameuonyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali.
Si mara nyingi hapa nchini utasikia tukiongelea ujasiri. Lakini namfikiria Lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi. Najua hivyo ndivyo alivyo. Waliomshambulia wamemuumiza. Wamemuumiza kweli. Na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri.
Alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu sio kitu rahisi kwa mtu yoyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumia moyo Sana kama asingesema maneno haya kwangu “tumeshinda. Tumeshashinda”.
No comments