Rais Shein ateua majaji wapya
Uteuzi wa wateule hao ulianza jana Ijumaa
Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 94(2) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais Shein amewateua Khamis Ramadhan Abdalla na Aziza Iddi Suweid kuwa majaji wa Mahakama hiyo.
Pia, amemteua Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa uwezo wake chini ya Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 4 ya 2015, kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 4 ya 2017, Kifungu cha 10(a)(1).
Katika uteuzi mwingine, Rais Shein amemteua George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anayeshughulikia masuala ya Katiba na Sheria.
Dk Shein chini ya kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya 1997, amemteua Kapteni Juma Haji Juma kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.
Taarifa ya uteuzi huo imesema ulianza jana Ijumaa.
No comments