OMMY DIMPOZ POLISI MASAA MATANO AKIHOJIWA
September 13, 2017 Mwimbaji wa BongoflevaOmmy Dimpoz alionekana kwenye kituo kikuu cha Polisi Kati Dar Es Salaam akiwa amesindikizwa na watu wengine wawili wakiingia kituoni hapo majira ya Asubuhi,Ommy Dimpoz alionekana akiingia kituoni hapo mida ya saa tano wakati waandishi wa habari walipokwenda kwenye press Conference ya kamanda wa Polisi Mambosasa.
Hata hivyo Kamanda MamboSasa kwenye taarifa yake ya mchana kwa waandishi wa habari hakuzungumzia ishu yoyote ya Ommy Dimpoz kuhojiwa lakini taarifa za chinichini ambazo hazijathibitishwa inasemekana Ommyaliitwa kuhojiwa na polisi ni kwa sababu ya ile picha aliyopost akiwa amepiga na mama mzazi wa Diamond.
No comments