MWIJAGE ASEMA INDIA IMEAHIDI KUJA KUWEKEZA TANZANIA
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya ziara yake nchini India.
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, leo amezungumzia ziara yake ya hivi karibuni nchini India ambapo alikwenda kwa ajili ya mkutano wa pamoja wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mwijage amesema ziara hiyo italeta manufaa makubwa kwa wafanyabiashara katika kukuza biashara kati ya Tanzania na India ambapo alisema wafanyakazi wa India watakuja nchini kwa ajili ya kuchunguza na kupata fursa za kuwekeza.
No comments