Breaking News

MBAO YAIVURUGA SIMBA


 

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea leo kwa mchezo mmojakati ya Mbao FC iliyowakaribisha wanamsimbazi Simba SC  katika uwanja wa CCM kirumba jijini mwanza. 

Mchezo umemalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2.

Simba walikuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 14 lililofungwa na Shiza kichuya, goli lililodumu kipindi chote cha kwanza. 

Kipindi cha pili kunako dakika ya 46, Habib Haji aliipatia Mbao bao la kwanza na kufanya matokeo kuwa 1-1.Muda mchache baadae katika dakika ya 47 James Kotei aliifungia Simba goli la pili.

Dakika ya 81, Emannuel Mbuyokole aliipatia Mbao goli la pili la kusawazisha na kufanya matokeo ya jumla kuwa 2-2. Full Time Mbao Fc 2-2 Simba SC

Kwa matokeo hayo Mbao FC imevuruga mipango ya Simba ya kukaa kileleni.Endapo Simba ingeshinda mchezo huo  ingekuwa na point 10 lakini  sasa ina point 8 na kushika nafasi ya pili ikiwa tayari imecheza michezo minne.

Mpaka sasa kinara wa Ligi ni Mtibwa Sugar yenye Point 9 ikiwa imecheza michezo mitatu

No comments