MADIWANI WAFUNGA BARABARA
Madiwani na wananchi wilaya ya Geita wamefunga barabara inayoingia mgodini kuzuia magari ya mgodi yasiingie hadi mgodi wa GGM mpaka walipe kodi Dola 12milioni wanazodaiwa.
Madiwani wa halmashauri mbili za wilaya ya Geita wamezuia magari ya mgodi kuingia au kutoka mgodini hadi watakapolipa kodi ya huduma wanayodai kuanzia mwaka 2003 hadi 2013
Ofisa uhusiano Mgodi huo Manase Ndoroma amesema wao wamelipa kihalali kwa mujibu wa sheria na kwamba kilichotokea ni migongano ya kisheria ambazo zote zimetungwa na bunge.
Polisi wameimarisha ulinzi katika maeneo ya Nungwe uliko mradi wa maji unaosambaza maji mgodini ,eneo la uwanja Wa Ndege na geti la kuingia mgodini ambako kote kuna askari wenye silaha.
No comments