TSHISHIMBI AFANYIWA MAZOEZI MAALUM
Njombe Mji inayonolewa na Kocha Hassan Banyai itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Sabasaba, Njombe.
Katika mchezo wa kwanza uwanjani hapo Njombe walifungwa mabao 2-1 na Prisons ya Mbeya.
Mmoja wa viongozi wa Njombe Mji ameliambia Championi Jumatatu kuwa, lengo la kujiandaa kuwazuia mastaa wa Yanga ni kuhakikisha wanaambulia hata pointi moja kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kama walivyofanya majirani zao Lipuli FC ya Iringa.
“Tunajua kuwa Yanga wana mastaa wanaofanya vizuri katika ligi akiwemo kiungo wao mpya, Papy Kabamba Tshishimbi lakini sisi nikwambie tu tunajiandaa vizuri kuhakikisha tunawazima hao na kutokuwa na madhara mbele yetu.
“Tumepania tupate hata pointi moja kwenye mechi hiyo kama lengo letu la pointi tatu litafeli, tunataka kuona tunafanya vizuri katika mchezo huo,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe
No comments