AZAM VS SIMBA VIINGILIO VYATANGAZWA
Shirikisho la Soka Tanzania limeweka wazi viingilio vya mechi ya Azam na Simba kuwa jukwaa kuu kiingilio kitakuwa Sh. 10000 ilihali majukwaa ya kawaida kiingilio ni Sh. 7000.
Timu hizo zitavaana Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kuchezwa usiku kwenye uwanja huo.
Ofisa Habari wa Azam, Japhar Idd aliwataka mashabiki wa soka kujitokeza mapema kununua tiketi za kushuhudia mchezo huo.
"Tunawakaribisha Chamazi mashabiki wote wanaotaka kushuhudia mechi hiyo, wawahi kununua tiketi mapema,"alisema Idd.
Katika mchezo huo Azam itashuhudia urejeo wa wachezaji wake waliohamia Simba msimu huu ambao ni nahodha wao wa muda mrefu John Bocco, Erasto Nyoni, Aishi Manula na Shomari Kapombe.
No comments