KABURI LA MWENDESHA BODABODA LAFUKULIWA NA POLISI
Moshi. Mwili wa dereva wa bodaboda, Juma Hamis (26) umefukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.
Hamis aliyekuwa mkazi wa Boma Mbuzi alizikwa katika makaburi ya Pasua mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kufukuliwa kwa mwili huo kunatokana na amri iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
Hamis alifariki dunia Julai 28 ikidaiwa ni kutokana na kipigo na kuzikwa Julai 29 katika makaburi ya Pasua.
No comments