Breaking News

Huyu ndo Jaji Jasiri Aliyebatilisha Uchaguzi wa Urais Kenya


Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi AgostiHaki miliki ya pichaEPA

Jaji wa makama ya juu David Maraga na wenzake wanne wameweka historia kwa kubatilisha uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti

Wakenya wamempongeza Jaji Maraga kwa kuwa jasiri kutengua uchaguzi wa mtu aliyemchagua rais Uhuru Kenyatta mbali na kurudisha imani katika idara ya huru wa mahakama.Magazeti kadhaa ya Kenya yamemtaja jaji Maraga kuwa mtu wa maadili kutokana na hatua yake ya kuwa muumini shupavu wa kanisa la Seventh Day.

Aliripotiwa akiliambia jopo lililokuwa likimhoji kwamba iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu nchini Kenya hatosimamia kesi siku ya Jumamosi , ambayo ni siku ya kupumzika kwa wanachama wa kanisa hilo.

Wengine wamedai kwamba huenda hii ndio sababu kikao cha kwanza cha kesi ya kupinga uchaguzi wa rais Uhuru Kenyatta kilianza mwendo wa saa moja usiku siku ya Jumamosi baada ya ya siku ya Sabato kuisha.

Imeripotiwa kuwa wakati alipokuwa akikaguliwa alikabiliwa na madai kwamba alikula hongo.
Aliwashangaza wengi kwa kutangaza katika runinga za taifa akiapa kwa kushikilia kitabu kitukufu cha Biblia kwamba hajawahi kuchukua hongo katika maisha yake.

Jaji Maraga mwenye umri wa miaka 66, alifuzu kama wakili miaka 40 iliopita kutoka chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuhudumu kama wakili wa kibinafsi.
Alichaguliwa jaji 2003 na kujiunga na mahakama ya rufaa 2012. Ameoa na ana watoto watatu.
Mwaka uliopita kufuatia kustaafu kwa jaji mkuu Willy Mutunga, aliwashinda majaji wengine 10, mawakili na wasomi kuteuliwa jaji mkuu.

Hatahivyo mapema mwaka huu aliripotiwa kumkemea mtu aliyemchagua, rais Uhuru Kenyatta.
Wakati akifanya kampeni nyumbani kwa jaji Maraga rais Uhuru Kenyatta alinukuliwa akisema kuwa wakaazi wa eneo hilo wanafaa kumpigia kura kwa sababu alimpatia kazi ''mwana wao''.
Hatahivyo jaji mkuu kupitia idara ya mahakama JSC alisema kuwa yeye sio mradi wa serikali.
Jaji Maraga na wenzake katika mahakama ya juu nchini KenyaHaki miliki ya pichaEPA

Jaji Maraga na wenzake katika mahakama ya juu nchini Kenya
Rais Uhuru Kenyatta hapo awali alikuwa amesema kuwa ataheshimu uamuzi wa mahakama , ijapokuwa alihoji ni kwa nini watu sita wanaweza kutoa uamuzi unaokwenda kinyume na matakwa ya Wakenya.
Hatahivyo baadaye alisema kuwa majaji hao walikuwa wamelipwa na ''watu wa kigeni pamoja na wajinga wengine''.

''Maraga na wahahalifu wake wameamua kubatilisha uchaguzi. Sasa mimi sio tena rais mteuliwa bali rais aliye mamlakani. Maraga anapaswa kujua kwamba sasa mimi ni rais anayehudumu''.
Licha ya vitisho hivyo , rais hana uwezo wa kumfuta kazi jaji mkuu ambaye muhula wake mmoja unakamilika wakati atakapofikisha miaka 70.


No comments