FAMILIA YA MTEKAJI WATOTO ARUSHA YASUSIA MAZISHI YA KIJANA WAO
Familia ya marehemu Samson Petro imefunguka na kusema haitofanya matanga wala kuufuata mwili wa marehemu kutokana na kitendo cha ukatili alichokifanya na kusema kuwa ni kitendo kisichoweza kuvumilika na wanaamini kuwa mwili huo haustaili kuzikwa.
Hayo yalizungumzwa na Petro Aaron, ambaye ni baba mzazi wa marehemu Samson mbele ya wanafamilia wengine akiwepo mama mzazi wa marehemu huyo, amesema kitendo kilichofanywa na marehemu si kitendo cha kusameheka wala kusahaulika katika jamii.
Marehemu Samson anatuhumiwa kwa kosa la utekaji na mauaji ya watoto wawili ambaye ni Moureen Njau na Ikhram Salim ambapo aliwaua na kuwatumbukiza katika mtaro wa maji machafu.
Aidha kamanda wa polisi mkoani Arusha , Charles Mkumbo ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa siku ya jumatano iliyopita na kutaka kutoroka ndipo polisi walipoamua kumjeruhi miguu yote miwili.
Kutokana na majeraha hayo, mtuhumiwa alipoteza damu nyingi na kumpelekea mauti kumkuta.
‘’ Mtuhumiwa alijaribu kutoroka, ndipo polisi walipolazimika kumjeruhi miguu yote miwili na kukimbizwa hopsitali ya Mkoa Mount Meru akibubujikwa na damu ndipo alipofariki dunia.
Tukio hilo lilitokea baada ya mtuhumiwa Samson, kukubali kuonesha eneo alilokuwa akiishi kijana mwingine aliyeshirikiana naye katika kufanya uhalifu huo.
No comments