Breaking News

DK BILAL ATOA ONYO KWA MAJANGILI


Kama nchi za Afrika hazitakuwa na mpango wa pamoja wa kupiga vita ya mauaji ya tembo na biashara ya pembe zake kuna hatari ya kutoweka kwa tembo hao

Makamu wa Rais Mstaafu Dk Mohamed Gharib Bilal amewataka watanzania kupambana  na watu wanaoharibu mazingira wakiwamo majangili.

Dk Bilal amezungumza hayo leo  alipokuwa kwenye uzinduzi wa Shirika la Waandishi wa Habari Marafiki wa Kupinga Ujangili na Mazingira jijini.

Bilali amesema watu wanaojihusisha na ujangili na biashara hiyo wanatakiwa kufichuliwa ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Amesema haiwezekani watu wachache waachiwe waendelee kuharibu  mazingira na kusababisha vizazi vyetu kukosa urithi wa asili wa maliasili.

“Hivyo kila mmoja wetu awe muhifadhi wa maliasili yetu kwa kuwa ni tunu zilizokuwa kwetu ili vizazi vijavyo viwezi kuvikuta ikiwemo wanyama pori ,uoto wa asili na mito,”amesema Dk Bilali.

Pia amesema chama hicho  kinatakiwa kupiga kelele ili kutokomeza ujangili na biashara haramu ambapo

wakifanikiwa watasaidia wanyama mbalimbali wakiwemo  tembo kuendelea kuwepo katika mbuga mbalimbali za nchini.

Amesema  hifadhi za wanyama zitakapoendelea kutunzwa watalii mbalimbali kutoka nje ya nchi wataingia nchini kufanya utalii.

Katibu wa Shirika hilo Sikwese Austin alisema taarifa ya ujangili kutoka Umoja wa Mataifa (UN recent report) inaonyesha kuwa tembo wenye asili ya Afrika idadi yake imepungua kutokana na ujangili kwa asilimia 30 kuanzia mwaka 2007 hadi 2014.

Austin amesema kama nchi za Afrika hazitakuwa na mpango wa pamoja wa kupiga vita ya mauaji ya tembo na biashara ya pembe zake kuna hatari ya kutoweka kwa tembo hao.

“Waathirika wakuu katika biashara hii haramu ni vijana wanatafuta maisha kwa njia ya mkato hutumiwa na vigogo wanaowarubuni kwa kiwango kidogo cha pesa na hatimaye wanapoteza maisha yao,”ameema Austin.

Amesema vita hiyo ni kubwa  inahitaji ushirikiano wa hali ya juu  hivyo wanawaomba wadau mbalimbali kuungana kwa pamoja ili kupiga vita biashara haramu ya meno ya .

Mwenyekiti wa shirika hilo ambaye ni Mbunge wa viti maalumu, Riziki Lulida alisema tembo ni mgodi unaotembea na hazina kuu katika kuingiza uchumi unaotokana na mapato ya utalii wa ndani ya nchi.

 “Msimamo wetu ni kuungana na serikali yetu kupiga vita biashara ya meno ya tembo pamoja na mauji ya tembo ndio maana nchi 29 zimedhamilia kukomesha biashara hii ikiwemo nchi ya Kenya imeonyesha mfano mzuri kuuthibiti ulimwengu kuwa haifiki biashara haramu nchini kwao.

No comments