Breaking News

CHANZO CHA NYUMBA YA ZITTO KUUNGUA CHATAJWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui 

Polisi wanasema kwamba wanamshikilia mlinzi wa Zitto Kabwe kwa mahojiano zaidi

4Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kuongezeka joto katika betri za sola ndio chanzo cha moto uliounguza Nyumba ya Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe jana jioni.

Nyumba hiyo ipo mtaa wa Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga katika wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.

Amesema  joto hilo limesababisha mlipuko wa moto kwenye betri za sola na hivyo nyumba kushika moto na kuteketea yote.

Polisi wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo, Norbert Joseph kwa mahojiano zaidi ili kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanywa na kusababisha moto kuwaka.

Msaidizi wa Zitto anayeifahamika kwa jina la  Nyembo Mustafa ametaja  thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo kwamba ni Sh 45 milioni.

No comments