Breaking News

WAHANDISI WA HABARI WASUBIRI KUAPISHWA

Zaidi ya Wahandisi 200 nchini wanatarajia kula kiapo cha utii kwa taaluma yao kitakachowaongonza kutokiuka miiko ya taaluma ya uhandisi kwa kuwajibika katika maamuzi yao na utendaji wao wa kazi sambamba na kufanya Umma ujenge imani kwa mhandisi mhusika husika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Msajili Bodi ya Usajili wa Wahandisi MhandisiPatrick Barozi amesema madhumuni ya kiapo hicho kwa wahandisi hao ni kumkumbusha mhandisi jukumu lake la kitaalamu na umuhimu wa kuzingatia taaluma wakati wote,kujenga imani kwa umma kwa mhandisi husika, kutumika dhidi ya mhandisi atakapovunja miiko ya taaluma katika utendaji wake wa kazi pamoja na kumlinda Mhandisi dhidi ya kulazimishwa kutenda mambo ambayo ni kinyume na taaluma yake.

Aidha Mhandisi Patrick Barozi amesema kuwa tendo hilo la kula kiapo cha utii kwa wahandisi hao litafanyika siku ya Wahandisi Tanzania 2017 itakayoadhimishwa tarehe 7 na 8 septemba 2017 mjini Dodoma ambapo katika madhimisho hayo mbali na tendo la kula kiapo kwa wahandisi mbalimbali pia shughuli mbalimbali za kiuhandisi zitafanywa ikiwemo maonyesho mbalimbali ya kiufundi na biashara.majadiliano ya kitaaluma pamoja na kuwatambua na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwaka wa mwisho 2016/2027.

No comments