Breaking News

VITA YA DIAMOND NA ALLY KIBA KUAMULIWA NIGERIA

Jana usiku majina ya wasanii waliochaguliwa kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za AFRIMA 2017 yametangazwa ambapo kwenye kipengele cha Msanii bora wa kiume kutoka Afrika Mashariki mahasimu Diamond Platnumz na Alikiba wamekutana tena kwenye kipengele hicho na ndiyo Wasanii pekee waliofanikiwa kuingia kwenye kipengele hicho.

Wasanii wengine kutoka Tanzania waliotajwa kwenye tuzo hizo ni Lady Jaydee, Nandy na Vanessa Mdee wote wapo kwenye kipengele cha msanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki.

Upigaji kura wa Tuzo hizo utaanza Tarehe 21 Agosti mwaka huu na zitatolewa tarehe 12 mwezi Novemba huko Lagos nchini Nigeria, Tazama Orodha kamili ya tuzo za AFRIMA 2017 hapa chini.

No comments