MECHI YA SIMBA NA SINGIDA KUPIGWA STOP SABABU HIZI HAPA
Mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Singida united uliopangwa kufanyika siku ya Jumapili Agosti 13 katika uwanja wa Taifa umeahirishwa.
Mchezo huo umeahirishwa kwa sababu Kesho Jumamosi kutakuwa na mchezo kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting hivyo serikali imekaa kuchezwa mechi mbili mfululizo katika uwanja huo wa Taifa.
Baada ya mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba na Yanga Agosti 23,uwanja wa Taifa utafungwa, nyasi zitan'golewa na kuwekwa mpya .Nyasi zilizowekwa wakati wa ujio wa EVERTON zilikuwa za kudumu kwa muda wa miezi miwili tu.
Kwahali hiyo Simba na Yanga zitatumia uwanja wa uhuru kwa michezo yake ya Ligi kuu mpaka pale uwanja wa Taifa utakapokuwa tayari
No comments