Breaking News

RC Mtwara 'amtumbua' kigogo wa ardhi

Na Yahya masangula

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amemsimamisha kazi mkuu wa idara ya ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Denis Kitali, kutokana na kukiuka makubaliano ya idara ya ardhi na ofisi ya mkuu wa mkoa juu ya namna bora ya kuuza viwanja 380 katika eneo la Msijute.

Akitangaza uamuzi huo katika kikao cha baraza maalum la madiwani la kujibu hoja za CAG, mkuu huyo wa mkoa amesema licha ya kusimamishwa kazi, hatua nyingine za kisheria zitafuata dhidi yake.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa amewataka baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo pamoja na viongozi wa kisiasa waliokula hela za watu kwa ajili ya zoezi la uuzwaji wa viwanja hivyo warudishe mara moja.

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo, akiwamo Maupa Abdul na Ramadhan Mfaume wameelekeza lawama zao kwa idara ya ardhi ya halmashauri hiyo kwa kutotimiza wajibu wao kikamilifu.

No comments